Ticker

6/recent/ticker-posts

punda milia


Punda milia au pundamilia ni wanyama wa familia Equidae wa Afrika wanaofahamika sana kwa rangi yao ya pekee ya michirizi myeupe na myeusi. Michirizi yao huwa na mpangilio tofauti kwa kila punda milia mmoja.

Ni wanyama wenye kuchangamana sana na huonekana mara nyingi kwenye makundi madogo na hata makubwa. Mbali na michirizi yao, punda milia wana nywele shingoni.

Tofauti na ndugu zao wa jirani, farasi na punda, pundamilia hajawahi kufugwa kwa mafanikio.

Kuna spishi tatu za punda milia: punda milia nyikapunda milia wa Grévy na punda milia milima, ambazo huainishwa zote kwenye nusujenasi Hippotigris. Zamani punda milia wa Grévy aliwekwa kwenye Delichohippus, lakini utafiti wa ADN umeonyesha kwamba ana uhusiano karibu na punda milia nyika. Kwa kweli, nusujenasi ya punda milia ina asili ya monofiletiki. Wanashiriki jenasi Equus na farasi na punda.

Upekee wa milia na tabia za pundamilia unawafanya kuwa miongoni mwa wanyama wanaofahamika sana kwa binadamu.

Pundamilia hupatikana katika maeneo mbalimbali, kama vile ukanda wa mbugasavana, ukanda wa misitu, kwenye vichaka vya miiba, milimani na kwenye vilima vya pwani.

Hata hivyo sababu mbalimbali za muingiliano wa jamii na tamaduni huleta athari kubwa katika idadi ya pundamilia, hasa kutafuta ngozi na uharibifu wa makazi. Grévy’s zebra na mountain zebra wapo hatarini kutoweka. Huku plains zebra wakizidi kuwa wengi, nususpishi moja, quagga, ilitoweka kabisa mwishoni mwa karne ya 19.

Jina la ‘zebra’ limetokana na neno la Kireno cha zamani, lisemalo ‘zeura’ likimaanisha punda wa porini