Ticker

6/recent/ticker-posts

sisimizi/ Ant


JE,WAJUA HILI?
Katika maisha ya sisimizi mda mwingi hutumia kufanya kazi.
Katika masaa 24(siku 1), sisimizi hulala dk16 tu. Yaani mchana anaweza lala dk8 na usiku anaweza lala dk8.
Hii hufanywa na wadudu wengi kama siafu

Sisimizi ni familia ya wadudu wadogo wanaoishi katika jamii. Jamii hizi zinaweza kuwa na sisimizi makumi kadhaa tu au kuwa na mamilioni kulingana na spishi mbalimbali.

Sisimizi jinsi anavyokamua vidukari

Makazi yao yapo mara nyingi chini ya ardhi au mahali pengine panapohifadhiwa kama chini ya jiwe kubwa au katika nafasi ndani ya miti. Wanatumia udongo na nyuzi za mimea kwa ujenzi.

Jenasi kadhaa kama vile siafu (Dorylus spp.) hawana makazi ya kudumu bali wanahamahama.

Mchwa hawako karibu na sisimizi hata kama wanafana nao katika mengi na kuitwa kwa Kiingereza "white ants" lakini wako katika nasaba nyingine pamoja na kombamwiko.